Timiza vikoba

You are here

1.TIMIZA VIKOBA NI NINI ?

Timiza Vikoba ni huduma za akiba na mikopo kwa vikundi kuanzia watu 5 hadi 50. Wanakikundi wanatakiwa kuweka akiba kwa wiki na haijalishi kama wana mkopo au la. Mikopo hii inatolewa kwa wanakikundi baada ya wiki nne ya kukusanywa kwa akiba kuzingatia mzunguko uliopo. Mkopo huu ni mara mbili ya salio la akiba ya kikundi. Akiba na mikopo hii hulipwa kupitia Airtel Money. Mwisho wa mzunguko wa kikundi, wanakikundi watapokea jumla ya akiba zao za wiki pamoja na riba.

2.NI VITU GANI MWENYEKITI WA KIKUNDI NA WANAKIKUNDI WANATAKIWA KUZINGATIA WAKATI WA KUSAJILI KIKUNDI?

  • Jina la kikundi – liwe limeunganishwa kama neno moja bila kuacha nafasi kati ya herufi
  • Namba ya siri ya kikundi – PIN, iwe yenye tarakimu nne
  • Idadi ya wanakikundi - (5-50)
  • Siku maalumu ya wiki ya malipo- kati ya (Jumapili – Jumamosi)
  • Kiasi cha akiba kwa wiki
  • Muda wa kikundi (miezi 6,9 au 12)
  • Muda wa mikopo ya TIMIZA VIKOBA ya kikundi (kuanzia wiki 4, 8, hadi 12).

3. JE, NITAHITAJI KUWA NA AKAUNTI YA BENKI ILI KUJIUNGA NA MKOPO?

Hapana. Ingawa utatakiwa kuwa na akaunti ya Airtel Money unayotumia. Utakapofungua akaunti ya Timiza Vikoba, hapohapo utafunguliwa akaunti ya akiba na Benki ya Maendeleo PLC.

4. NINAWEZA KUPATA MIKOPO MINGAPI KWA WAKATI MOJA?

Utaweza kupata mkopo mmoja tu kwa mara moja. Baada ya mkopo wako kulipwa, utapatiwa nafasi ya mkopo mwingine.

5. MKOPO WA TIMIZA VIKOBA UNA GHARIMU KIASI GANI CHA RIBA?

Riba ya mikopo ya TIMIZA VIKOBA ni 4% kwa mwezi

6.JE, NI NINI KITATOKEA KAMA NIKICHELEWA KUWEKA AKIBA YA WIKI AU KUREJESHA MALIPO YA MKOPO?

Ikitokea umechelewa kuweka akiba ya wiki au kurejesha malipo ya mkopo, utatozwa kila siku kwa malimbilkizo ya hadi siku tatu. Wanakikundi wote pia watataarifiwa kuwa unadaiwa. Baada ya siku ya tatu, kikundi chako kitaorodheshwa kama kikundi kisicho shirikishi na hakuna mwanakundi atakayeweza kupata mkopo wowote hadi marejesho yatakapofanyika

7.NINI HATIMA YA KUNDI AMBALO ‘SIO SHIRIKISHI’?

Ikitokea kikundi kikaorodheshwa kama kikundi ambacho si shirikishi, ni jukumu la mwenyekiti wa kikundi (na wanakikundi wote) kushirikiana katika kumhimiza mwanakikundi anayedaiwa kutimiza wajibu wake kabla kundi zima halijaathirika. Kama kikundi kitabaki kuwa sio shirikishi kwa muda wa siku 7, hapohapo kitavunjwa na kutotambulika kwenye mfumo. Tozo na madeni yoyote yaliyobaki yatalipwa kwa kukatwa kwenye kila akiba ya dhamana ya mwanakikundi. Ikitokea akiba ya dhamana ya mwanakikundi haitoshelezi kufidia deni lao, akiba ya dhamana ya wanakikundi wengine zitatumika kufidia kiasi husika. Kiwango cha akiba baada ya tukio hilo kitarudishwa kwenye akaunti ya Airtel Money ya kila mwanakikundi. Kikundi kitakachofungiwa mapema hakitalipwa riba yoyote kwenye akiba yao.

8.JE NITARUDISHIWA AKIBA YANGU YA DHAMANA?

Ndio, kikundi chako kitakapofika mwisho wa mzunguko wake, na marejesho yote ya mikopo kufanyika, utarudishiwa jumla ya akiba yako ya dhamana pamoja na riba. Akiba ya dhamana haiwezi kutolewa kabla ya mwisho wa mzunguko wa kikundi labda hicho kikundi kivunjwe kabla ya mzunguko kuisha.

9.NITAINGIZA KIASI GANI CHA RIBA?

Riba itakayolipwa kwa akiba ya dhamana ni kiasi cha 2% kwa mwaka.

10.MIKOPO HUKUCHUA MUDA GANI?

Mikopo hulipwa ndani ya wiki 4, wiki 8 au wiki 12. Marejesho ya mikopo ni kila wiki ikitegemea siku iliyochaguliwa na wanakikundi.

11.VIPI KAMA NATAKA KULIPA MAPEMA?

Unaweza kulipa deni lako muda wowote, hata kabla ya muda. Ili kulipia mapema deni lako, akiba yako ya wiki ni lazima iwe imeshalipiwa hadi wiki hiyo. Baada ya hapo, unaweza kulipia kiasi cha deni kilichopo na malipo hayo yatatumika kulipia mapema deni lililopo. Baada ya kulipia mkopo wako mapema, utapata nafasi ya kupewa mkopo mwingine kama unastahili.

12.NI VIGEZO GANI VITANIWEZESHA KUPATA MKOPO MKUBWA?

Tafadhali endelea kulipa akiba ya dhamana kama inavyotakiwa kila wiki. Kwakuwa mkopo unaotolewa ni mara mbili ya akiba yako, kila nafasi mpya ya mkopo itakayotolewa huwa inaongezewa thamani kuliko ya wiki iliyopita. Salio lako la akiba ya dhamana huongezeka wiki hadi wiki.

13.Hatua zipi zitachukuliwa kwa wadaiwa wasiorejesha mikopo?

Endapo akiba ya dhamana haitotosheleza kulipia deni la mdaiwa, mdaiwa ataombwa kumalizia kiasi kilichobaki. Mdaiwa pia anaweza kushtakiwa na kuorodheshwa kwenye taasisi mbalimbali za kibenki Tanzania

13.HATUA ZIPI ZITACHUKULIWA KWA WADAIWA WASIOREJESHA MIKOPO?

14. MTEJA ATAPATA VIPI MSAADA KAMA TATIZO KUHUSU HUDUMA YA TIMIZA VIKOBA LINAPOTOKEA ?

Mteja atahudumiwa kwa kupiga namba 100 huduma kwa wateja bure

 

 

P. O. Box 216 Dar es salaam Tel : +255 22 2110518 Fax : +255 22 211 595 Email : info@maendeleobank.co.tz