loader image

Maendeleo Bank PLc

Mobile Menu

Maendeleo Bank Plc Yazindua Mtandao wa Biashara Kupitia SME Clinic

Maendeleo Bank Plc imeendelea kuthibitisha nafasi yake kama benki rafiki wa wafanyabiashara kwa kuzindua rasmi Maendeleo Bank Growth Network (MBGN) kupitia jukwaa la SME Clinic. Uzinduzi huu umefanyika katika kikao maalum kilichokutanisha wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs) pamoja na wadau wa kifedha na kibiashara.

 

SME Clinic ni jukwaa linaloandaliwa na Maendeleo Bank kwa ajili ya kuwakutanisha wafanyabiashara na kuwapa nafasi ya kupata ushauri wa kitaalam, elimu ya kifedha, na mbinu za ubunifu katika uendeshaji wa biashara zao. Ndani ya kikao hiko, benki imezindua mtandao mpya wa kibiashara – MBGN – ambao utakuwa chombo mahususi cha kuwaunganisha wateja, kuimarisha ushirikiano, na kufungua fursa mpya za masoko.

Kupitia MBGN, wafanyabiashara waliohudhuria SME Clinic watapata manufaa kama:

  • Mitandao ya kibiashara (Business networking) – kujenga mahusiano na kushirikiana na wafanyabiashara wengine.
  • Mafunzo na uelewa wa kifedha – kupitia semina za mara kwa mara.
  • Ushauri wa kibiashara – kupata msaada wa kitaalam juu ya changamoto za biashara.
  • Fursa za masoko – kutambulishwa kwenye majukwaa mapya na kushiriki fursa za ushirikiano.

Akizindua rasmi mtandao huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Plc, Ndugu Lomnyaki Saitabau, alisema kuwa benki imejipanga kuhakikisha wafanyabiashara, hususani SMEs, wanapata suluhisho la kifedha na huduma rafiki zinazojibu changamoto zao za kila siku.

Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Plc, Ndugu Lomnyaki Saitabau

“Tunataka wafanyabiashara wetu wajue kwamba hawako peke yao. Maendeleo Bank PLC ipo pamoja nao, si tu kama benki, bali kama mshirika wa karibu wa safari yao ya kibiashara,” alisema Ndugu Lomnyaki Saitabau kwa msisitizo.

Mkuu wa Idara ya Biashara, Ndugu Emmanuel Mwaya,

Akizungumza na washiriki, Mkuu wa Idara ya Biashara, Ndugu Emmanuel Mwaya, aliwahimiza wafanyabiashara kutumia kikamilifu huduma za benki ili kunufaika nazo, ikiwemo huduma za bima, internet banking, na mobile app ambazo zimeundwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha.

Aidha, washiriki walipata fursa ya kujifunza mbinu mbadala za kukuza biashara kupitia mada iliyowasilishwa na Ndugu Erick Chrispine kutoka True Maisha, aliyegusia njia bora za ubunifu na uthubutu katika uendeshaji wa biashara.

 

 

Scroll to Top