Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Alex Malasusa, leo Jumanne Februari 24, 2026 amezindua rasmi tawi jipya la Maendeleo Bank PLC jijini Arusha. Hili ni tawi la sita la Benki yetu na la kwanza kufunguliwa nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank PLC, Bw. Lomnyaki Saitabau, amesema kuwa tawi hilo linaenda kuleta mageuzi katika huduma za kifedha jijini Arusha kwa kutoa elimu ya kifedha pamoja na huduma jumuishi za kifedha kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa Arusha na mikoa jirani.

Pamoja na hilo Mkurugenzi Mtendaji Bw. Lomnyaki Saitabau ameeleza kuwa tawi hili litahudumia taasisi zote za kidini, Dayosisi za KKKT, taasisi zote zilizo chini ya KKKT na watu wote huku ikitoa huduma jumuishi kwa makundi yote kuanzia mtu binafsi, vikundi, kampuni, wajasiliamali, watoto, familia na watu wote kutoka katika Mkoa wa Arusha na maeneo ya jirani.





