loader image

Maendeleo Bank PLc

Mobile Menu

Maendeleo Bank PLC sasa ni Benki ya Kibiashara ya Kitaifa

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, leo Julai 3, 2025, ameizindua rasmi Maendeleo Bank PLC kuwa Benki ya Kibiashara ya Kitaifa.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maendeleo Bank PLC kuwa Benki ya Kibiashara ya Kitaifa, Mgeni Rasmi,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa,ameipongeza Maendeleo Bank PLC kwa hatua hiyo itakayowezesha kuwafikia Watanzania wengi zaidi nchini na kuwainua kiuchumi.

 

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank PLC Bw.Lomnyaki Saitabau akimkaribisha mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa Maendeleo Bank PLC kuwa Benki ya Kibiashara ya Kitaifa, pamoja na uzinduzi wa MB Mobile App na Mpango Mkakati (2025-2030)

 

 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Hamad H. Chande akitoa pongezi kwa mafanikio makubwa kwa Maendeleo Bank kwa kipindi chote tangu kuanzishwa kwake.
Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Mchungaji Chediel Lwiza akiwasilisha neno la pongezi kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa kwa mafanikio makubwa ya Benki.

Pamoja na uzinduzi wa kuwa Benki rasmi ya Kitaifa ya kibiashara, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, alizindua huduma ya MB Mobile App pamoja na Mpango mkakati wa Benki katika kipindi cha 2025-2030.

 

Katika siku hiyo Maendeleo Bank PLC tulimkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa tuzo ya kuonesha shukrani zetu kwa jinsi serikali inavyofanya kazi kuweza kuwaletea maendeleo wananchi pamoja na kuboresha huduma za kifedha nchini.

Scroll to Top