TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA SITA WA MWAKA:
Taarifa inatolewa kwamba Mkutano
Mkuu wa SITA wa Mwaka wa Wanahisa wa Maendeleo Bank PLC utafanyika Jumamosi
tarehe 27 Juni 2020 kuanzia SAA NNE ASUBUHI na wanahisa watashiriki Mkutano huo
kwa njia ya MTANDAO wa Zoom.
Mkutano Mkuu wa mwaka utafanyika
kwa njia ya mtandao ili kuepuka uwekano wa maambukizi ya ugonjwa wa Corona
kutokana na idadi kubwa ya Wanahisa wanaotegemewa kuhudhuria na kukosekana kwa
Ukumbi mkubwa wenye uwezo wa kukaa kwa kuzingatia taratibu na ushauri wa
madaktari unaotaka watu kutokaribiana na kupeana nafasi ili kujikinga dhidi ya
maambukizi. Benki inachukulia kwa makini usalama na afya za Wanahisa Pamoja na
wadau wake wote. Benki inaunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali
kupambana na ugonjwa huu hatari wa Corona kwa kufuata taratibu zote za kiafya
zinazosisitizwa na wataalamu ikiwemo; kuepuka mikusanyiko na watu kutosongamana
na kuachiana nafasi angalau mita moja kati ya mtu na mtu.
Agenda zitakuwa kama ifuatavyo:
1. Kufungua Mkutano.
2. Kuridhia Ajenda za Mkutano
Mkuu wa Sita wa Mwaka.
3. Azimio Maalum kuidhinisha
marekebisho kwenye Katiba ya Benki (MEMARTS) kuruhusu Mkutano Mkuu kufanyika kidijitali.
4. Kupitia na kuthibitisha
Kumbukumbu za Mkutano Mkuu wa Tano.
5. Yatokanayo na Mkutano Mkuu wa
Tano.
6. Kupokea na Kuridhia Taarifa ya
Wakurugenzi.
7. Kupokea Taarifa ya Hesabu
zilizokaguliwa za Mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2019.
8. Kupokea na Kuidhinisha Malipo
ya Wakurugenzi wa Bodi kwa Mwaka 2020.
9. Kuteua Mkaguzi Huru wa Hesabu
kwa Mwaka utakaoishia tarehe 31 Desemba 2020
10. Kupokea na Kuidhinisha
Pendekezo la Gawio.
11. Mengineyo kwa idhini ya
Mwenyekiti
12. Kupendekeza Tarehe ya Mkutano
Ujao.
13. Kufunga Mkutano.
MAMBO YA KUZINGATIA:
1. Mwanahisa atakayetaka
kushiriki katika Mkutano Mkuu utakaofanyika kwa njia ya mtandao, atatakiwa
kuthibitisha ushiriki wake kwa kutoa taarifa kwa katibu wa Kampuni kwa njia ya
barua pepe kupitia shareholders@maendeleobank.co.tz au ujumbe mfupi wa simu/whatsapp namba 0677-500050 kuanzia tarehe 20
Juni 2020 ili kupata maelekezo na kiunganishi cha mkutano.
2. Mwanahisa yeyote anayestahili
kushiriki kwenye Mkutano Mkuu au kuteua mwakilishi. Wanahisa wanaotaka kutuma
wawakilishi, wanaombwa kujaza fomu ya uwakilishi (proxy) inayopatikana kwenye
mtandao wa benki (www.maendeleobank.co.tz). Fomu ya uteuzi itume kwa njia ya
barua pepe au whatsapp namba 0677500050 siku moja kabla ya Mkutano.
3. Taarifa ya Mwaka 2019 na
Makabrasha ya Mkutano yatapatikana kwenye tovuti ya Benki (www.maendeleobank.co.tz)kuanzia
tarehe 15 Juni 2020.
4. Mapendekezo ya Wanahisa
yatakayojadiliwa katika agenda namba 11 yawasilishwe kwa Katibu kwa njia ya
barua pepe kwenda shareholders@maendeleobank.co.tz au ujumbe mfupi wa
simu/whatsapp namba 0677-500050 kabla ya tarehe 25 Juni 2020 saa kumi jioni.
Bonyeza
hapa kupakua fomu ya uwakilishi
KWA IDHINI YA BODI
DR. IBRAHIM MWANGALABA
MKURUGENZI MTENDAJI NA KATIBU
WA BODI
Tarehe 04 Juni, 2020