Maendeleo Bank ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dr. Ibrahimu Mwangalaba leo tumefanya zoezi la kufanya usafi katika eneo la Kivukoni (Ferry) jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya shughuli za kijamii katika kusheherekea kutimiza miaka saba kwa Bank yetu.

 

 

Pamoja na usafi huu, Maendeleo Bank imekabidhi vifaa mbalimbali vya usafi kwa ajili ya kutunza mazingira katika kivuko na sehemu mbalimbali za Ferry jijini Dar es Salaam, vifaa hii vimepokelewa na mamlaka ya Soko la Ferry na Meneja Dennis Mrema.

 

 

Pamoja na usafi, Mkurugenzi Mtendaji Dr. Mwangalaba alitumia nafasi hii kuwakaribisha wafanyabiashara wadogo wadogo wanaofanya shughuli zao katika soko la Ferry kuitumia Maendeleo Bank kujipatia mikopo isiyo nadhamana illi kuweza kukuza na kuendeleza biashara zao.