Leo tarehe 13-07-2020 Mkurugenzi Mtendaji Dr. Ibrahim Mwangalaba pamoja na wafanyakazi wa Maendeleo Bank kwa pamoja  tulikuwa Kanisa la KKKT Usharika wa Sinza kwa ajili ya ibada maalumu ya kumshukuru Mungu kwa kufikisha miaka 7 ya kutoa huduma za kibenki.

Ibada hii iliongozwa na Dean Chediel Lwiza. 

Maendeleo Bank tunayo furaha kubwa na kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa hatua hii tuliyoifikia kwa kuendelea kutoa huduma bora za kibenki kwa watanzania wote.