TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA NANE WA MWAKA:
Taarifa inatolewa kwamba Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Maendeleo Bank PLC utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 25 Juni 2022 katika ukumbi wa Msasani Tower, Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Ajenda za Mkutano ni:
1. Kufungua Mkutano
2. Kupokea na Kupitisha Ajenda za Mkutano Mkuu wa 8 wa Mwaka
3. Kupitia na Kuthibitisha Kumbukumbu za Mkutano Mkuu wa 7 wa Mwaka
4. Yatokanayo na Mkutano Mkuu wa 7 wa Mwaka
5. Taarifa ya Wakurugenzi kwa Mwaka Ulioishia tarehe 31 Disemba 2021
6. Taarifa ya Mkaguzi wa Nje na Taarifa za Fedha Zilizokaguliwa kwa Mwaka Ulioishia tarehe 31 Disemba 2021
7. Kupokea na Kuidhinisha mapendekezo ya Posho na Ada za Wakurugenzi kwa Mwaka 2022
8. Kupokea na Kuidhinisha Mapendekezo ya Mkaguzi wa Nje kwa Mwaka Utakaoishia Tarehe 31 Disemba 2022
9. Kupokea na Kuidhinisha Pendekezo la Gawio
10. Mengineyo
11. Kupanga Tarehe ya Mkutano Mkuu wa Mwaka Ujao
12. Kufunga Mkutano
ZINGATIO:
1. Mwanahisa anayetaka kuhudhuria mkutano atajigharamia mwenyewe na anapaswa kuja kwenye mkutano
akiwa na cheti cha Hisa na kitambulisho chenye picha kwa ajili ya utambulisho.
2. Mkutano pia utafanyika kwa njia ya mtandao wa zoom anuani ya mkutano itatumwa kwenye barua pepe
au namba ya simu ya Mwanahisa iliyosajiliwa Benki. Hivyo wanahisa wanaopendelea kuhudhuria mkutano
huu kwa njia ya mtandao wa zoom, wawasiliane na Katibu wa Benki kupitia barua pepe: shareholders@
maendeleobank.co.tz au ujumbe wa simu / WhatsApp kupitia +255677 500050 hadi 24 Juni 2022 ili
kupata taarifa na muongozo wa namna ya kushiriki kwenye mkutano huu.
3. Nakala za vitabu vya Mkutano Mkuu na fomu za uwakilishi zitapatikana Makao Makuu ya benki yaliyopo
Luther House, Barabara ya Sokoine, kuanzia tarehe 15 Juni, 2022, na pia vitabu vitapatikana ukumbini hiyo
tarehe 25 Juni 2022 au inaweza kupakuliwa kutoka kwenye tovuti ya benki, www. maendeleobank.co.tz
kuanzia tarehe 15 Juni 2022.
4. Mwanahisa anayestahili kuhudhuria Mkutano na ambaye ataona kwamba hataweza kuhudhuria yeye
mwenyewe, anatakiwa kumteua Mwakilishi wake kwa kujaza fomu za uwakilishi na kuziwasilisha zikiwa
zimetiwa saini na kubandikwa stempu za ushuru za TZS 500 na zifikishwe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Maendeleo Bank PLC, saa 48 kabla ya tarehe ya Mkutano. Ikiwa Mwanahisa ni kampuni, fomu ya mwakilishi
lazima iwe na lakiri ya kampuni aje akiwa na cheti cha Hisa.
5. Mapendekezo yoyote ya Wanahisa yapelekwe/yatumwe kwa Katibu kupitia barua pepe shareholders@
maendeleobank.co.tz au WhatsApp namba +255677500050 saa 48 kabla ya tarehe ya Mkutano.
PAKUA MKUTANO MKUU WA NANE WA MAENDELEO BANK PLC WA WANAHISA
KWA AGIZO LA BODI
DR IBRAHIM MWANGALABA
25 May 2022