Uzinduzi wa Maendeleo Bank Marathon “Hatua ya Faraja Msimu wa Pili “
Maendeleo Bank PLC leo Agosti 02,2024 tumefanya uzinduzi wa 𝐌𝐚𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐨 𝐁𝐚𝐧𝐤 𝐌𝐚𝐫𝐚𝐭𝐡𝐨𝐧 Hatua ya Faraja Msimu wa Pili itakayofanyika Septemba 07,2024 katika viwanja vya Farasi,Oysterbay
Uzinduzi huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Maendeleo Bank PLC Prof. Ulingeta Obadia Mbamba,akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji CPA.Peter Tarimo na Mkurugenzi Mtendaji Mstaafu wa Maendeleo Bank PLC Dkt.Ibrahim Mwangalaba.
Baada ya uzinduzi huo ambao uliambatana na kutambulisha jezi mpya,tulifanya mbio fupi zenye shamrashamra kutoka Makao Makuu ya Maendeleo Bank PLC Luther House-Posta mpaka viwanja vya Farasi,Oysterbay