Maendeleo Bank PLC sasa ni Benki ya Kibiashara ya Kitaifa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, leo Julai 3, 2025, ameizindua rasmi Maendeleo Bank PLC kuwa Benki ya Kibiashara ya Kitaifa. Pamoja na uzinduzi wa kuwa Benki rasmi ya Kitaifa ya kibiashara, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, alizindua huduma ya MB Mobile App pamoja na Mpango mkakati wa Benki katika kipindi cha 2025-2030. Katika siku hiyo Maendeleo Bank PLC tulimkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa tuzo ya kuonesha shukrani zetu kwa jinsi serikali inavyofanya kazi kuweza kuwaletea maendeleo wananchi pamoja na kuboresha huduma za kifedha nchini.
