loader image

Maendeleo Bank PLc

Mobile Menu

Event & News

Enter News and Event

Event & News, latest_news

Maendeleo Bank PLC sasa ni Benki ya Kibiashara ya Kitaifa

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, leo Julai 3, 2025, ameizindua rasmi Maendeleo Bank PLC kuwa Benki ya Kibiashara ya Kitaifa.         Pamoja na uzinduzi wa kuwa Benki rasmi ya Kitaifa ya kibiashara, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, alizindua huduma ya MB Mobile App pamoja na Mpango mkakati wa Benki katika kipindi cha 2025-2030.   Katika siku hiyo Maendeleo Bank PLC tulimkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa tuzo ya kuonesha shukrani zetu kwa jinsi serikali inavyofanya kazi kuweza kuwaletea maendeleo wananchi pamoja na kuboresha huduma za kifedha nchini.

Event & News

Mkurugenzi Mtendaji aanza kazi rasmi

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Maendeleo Bank PLC Mr. Lomnyaki Saitabau ameanza kazi rasmi leo baada ya utambulisho rasmi uliotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo Bank PLC Prof. Ulingeta Obadia Mbamba. Katika tukio hilo la kihistoria, Mr.Lomnyaki Saitabau alipata fursa ya kuzungumza moja kwa moja na wafanyakazi wa Maendeleo Bank,akiwashukuru kwa ukaribisho wao na kuahidi kushirikiana nao kwa bidii ili kuendeleza mafanikio ya benki yetu.

Scroll to Top