loader image

Maendeleo Bank PLc

Mobile Menu

Mkurugenzi Mtendaji aanza kazi rasmi

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Maendeleo Bank PLC Mr. Lomnyaki Saitabau ameanza kazi rasmi leo baada ya utambulisho rasmi uliotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo Bank PLC Prof. Ulingeta Obadia Mbamba.

Katika tukio hilo la kihistoria, Mr.Lomnyaki Saitabau alipata fursa ya kuzungumza moja kwa moja na wafanyakazi wa Maendeleo Bank,akiwashukuru kwa ukaribisho wao na kuahidi kushirikiana nao kwa bidii ili kuendeleza mafanikio ya benki yetu.

 

Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Maendeleo Bank, CPA Peter Tarimo,akitoa pongezi zake za dhati kwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Maendeleo Bank PLC,Lomnyaki Saitabau

Katika hotuba yake, CPA Peter Tarimo aliishukuru timu ya Maendeleo Bank PLC kwa ushirikiano wa kipekee wakati wa uongozi wake wa muda na kumtakia Mr.Lomnyaki Saitabau kila la heri katika safari yake ya kuongoza benki yetu kuelekea mafanikio makubwa zaidi.

Mchungaji Charles Mzinga wa KKKT- Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Azania Front akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Maendeleo Bank PLC,Mr.Lomnyaki Saitabau ambaye leo amekaribishwa na kuanza kazi rasmi.

 

More Updates

Scroll to Top