Mkurugenzi Mtendaji aanza kazi rasmi
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Maendeleo Bank PLC Mr. Lomnyaki Saitabau ameanza kazi rasmi leo baada ya utambulisho rasmi uliotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo Bank PLC Prof. Ulingeta Obadia Mbamba. Katika tukio hilo la kihistoria, Mr.Lomnyaki Saitabau alipata fursa ya kuzungumza moja kwa moja na wafanyakazi wa Maendeleo Bank,akiwashukuru kwa ukaribisho wao na kuahidi kushirikiana nao kwa bidii ili kuendeleza mafanikio ya benki yetu.

